Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania Jimmy Masaoe
Na Magreth Katengu - Dar es salaam
Serikali imedhamiria kukuza tasnia ya michezo kwa kuwapatia wadau mbalimbali ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kutambulisha kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubahatisha Betway, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Addo Kombo amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni kama Betway wa kuendeleza tasnia ya michezo.
Ameongeza kuwa serikali imejipanga kuboresha tasnia ya michezo ambapo imetenga bajet ya Tsh Bilion 10.5 ya kujenga vituo vitatu vya Michezo katika mikoa ya Dar es salaam,Dodoma na Geita.
"Pia serikali imetenga Bilion 1.5 kwa ajili ya kujenga kituo cha mafunzo ya maendeleo nchini na wadau watanufuika zaidi", alisema Addo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza la michezo nchini (BMT) Neema Msithe ameziomba kampuni za michezo zinazowekeza nchini kuwasaidia wachezaji wastaafu kwa kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali wanazozifanya kutokana wengine baada ya kustaafu wana hali mbaya kiuchumi.
Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania Jimmy Masaoe amesema mbali ya kutoa burudani ya kusisimua uwanjani pia wana mipango ya kusaidia jamii nje ya uwanja na nia ya maendeleo michezo kwa kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.
"Ni wakati mzuri katika sekta ya michezo ya kubashiri tunaamini kwa uzinduzi wa bidhaa hii yenye ubora wa kimataifa kwenye soko tunaweza kuleta msisimko kwa mashabiki wakati bado tunarudisha kwa jamii kupitia miradi mbalimbali ya michezo",alisema jimmy
Social Plugin