Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA CRDB AKIFUNGA MAONESHO SHINYANGA


Kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimuelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (katikati) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB zikiwemo huduma za Bima, Mikopo na Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) alipotembelea Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) alipotembelea Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akishuhudia shughuli za kibenki ikiwemo kufungua akaunti na kutoa fedha zikiendelea kwenye Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga ambapo alisema Benki ya CRDB inatoa huduma za mikopo hivyo wachimbaji wa madini na wajasiriamali wachangamkie fursa hiyo.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akimkabidhi Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui (kulia) cheti cha utoaji huduma bora wakati wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui ambao ni miongoni mwa Wadhamini wakuu wa Maonesho hayo akionesha zawadi aliyopewa na Kamati ya Maonesho wakati wa ufungaji wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com