Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati amezuia zaidi ya tani 400 za dengu zinazodaiwa kununuliwa kutoka kwa wakulima kwa njia ya ulanguzi zisisafirishwe nje ya mkoa huo.
Dkt. Sengati ameagiza shehena hiyo ambayo ilikuwa imepakiwa kwenye malori tayari kwa kusafirishwa, ishushwe na kuhifadhiwa kwenye magala ya Vyama vya Msingi vya Ushirika (Amcos) na Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (Shirecu) kusubiri mnada.
Via Mwananchi
Social Plugin