Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imetoa amri ya kuzuia mnada wa mazao ya dengu uliopangwa kufanyika kesho tarehe 27/8/2021 katika maghala ya SHIRECU.
Mahakama Kuu imetoa zuio hilo dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Chama Cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU).
Amri hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Philemon Sengati kukamata zaidi ya tani 400 za dengu za wafanyabiashara mbalimbali mkoani Shinyanga wakiongozwa na kampuni ya Afrisian.
Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 1/9/2021
Social Plugin