Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

EWURA YAFUNGIA VITUO 26 VYA MAFUTA

 

Na Magrethy Katengu - Dar es salaam

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  imevifungia vituo ya Mafuta 26 na kuvitoza faini kwa kosa la kukwepa kodi kwa kukutwa na mafuta yasiyokidhi viwango vya vina saba.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Godfrey Chibulunje amesema zoezi la ukaguzi lilianza julai 2 mwaka huu na lilifanyika katika mikoa ya kanda ya mashariki (Dar es salaam na Pwani ,kanda ya Ziwa ,kanda za juu kusini ,kanda ya kati ambapo hadi kufikia agosti 9 mwaka huu 

Sanjari na hayo amesema jumla ya vituo 195 vilikaguliwa ambapo vituo 26 sawa asilimia 13.33 vilikutwa na mafuta ambayo hayana kiwango stahiki cha vinasaba ikiwemo Lake oil Company cha Geita,GBP Oill  Mwanza, Total Tanzani Mwanza,Azhad Abdulrahim Mkuranga ,Ally Adon ya Mombasa.

“Kwa mujibu wa kanuni kampuni zenye depots zinatakiwa kuhakikisha mafuta yote yaliyonunuliwa kwa ajili ya soko la ndani yanawekewa  vinasaba na Mfanyabiashara yeyote anayenunua mafuta anatakiwa kuhakikisha yanawekwa vinasaba kwa usahihi kwenye gari likilobeba mafuta" amesema Chibulunje.

Hata hivyo amesema baada ya TBS kukabidhi EWURA  mashine za kung’amua vinasaba kwenye mafuta (Fuel marker dectection machine )ilianza zoezi la ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuhakiki kama mafuta kwenye vituo hivyo yana kiwango sahihi cha vvinasaba

Aidha EWURA imewaasa Wafanyabiashara wote kufanyabiashara zao kwa kufuata taratibu za sheria zilizowekwa ili kuepuka usumbufu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com