Mbunge wa Muheza, Hamis Mwijuma maarufu kama Mwana FA amepata ajali katika eneo la Mkambarani mkoani Morogoro baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na gari ndogo aina ya Toyota Crown iliyokuwa ikijaribu kulipita gari lake wakiti akitoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
Watu wawili ambao walikuwa ni abiria kwenye gari aina ya crown wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa, Morogoro, kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mororgoro, Fortunatus Musilim.
“Ni kweli Mhe. Mbunge amepata ajali, ila yuko salama. Amepata ajali majira ya saa mbili usiku baada ya gari aina ya Toyota Crown iliyokuwa na abiria wanne kujaribu kuipita gari yake,” amesema Musilim.
“Hata hivyo Mhe. Mbunge alitumia gari lake kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Mkoa,”
Musilim amesema watu wengine wawili waliokuwa kwenye Crown walipata michubuko kadhaa na wako salama.
Chanzo - GlobalTVOnline
Social Plugin