Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
**
Wakati mjadala wa sharti la cheti cha ndoa kwenye fumanizi ukishika kasi, imeelezwa kuwa zipo ndoa hazina vyeti na zinatambulika kisheria, lakini wengi hawana uelewa huo.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria wamewashauri watu badala ya kufumania, kufungua kesi ya madai na kumdai fidia kiasi chochote mtu mwenye uhusiano na mwenza wake.
Juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene alisema, “itahesabiwa fumanizi hadi pale huyo anayefumaniwa, iwe mwanamke au mwanaume awe na cheti cha ndoa halali. Sio mtu alikuwa rafiki yako kwa muda, wewe bado unatafuta uhalali wa kuonekana unammiliki, unamvamia na kurekodi picha kisha kusambaza.”
Via Mwananchi
Social Plugin