Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BONDIA YORDENIS UGAS AMTEMBEZEA KICHAPO MANNY PACQUIAO


Bondia Yordenis Ugas akikabidhiwa mkanda kwenye pambano la mkanda wa uzito wa juu wa WBA 'super' middleweight.

***
Bondia Manny Pacquiao amepoteza pambano dhidi ya Bondia Yordenis Ugas aliyechukua nafasi ya Errol Spence Jr, kwa tofuti ya alama kwenye pambano la mkanda wa uzito wa juu wa WBA 'super' middleweight.

Manny Pacquiao raia wa Ufilipino alipoteza pambano hilo kupitia uamuzi wa alama katika pambano ambalo linatajwa huenda likawa la mwisho la bondia huyo mwenye umri wa miaka 42.

Ugas raia wa Cuba mwenye umri wa miaka 35 alitumia vizuri fursa aliyoipata baada ya kuumia kwa Errol Spence Jr na yeye kupewa nafasi ya kua mpinzani wa Pacquiao.

Licha ya kurusha makonde machache kuliko Pacquiao, lakini mapigo ya Ugas yalikuwa sahihi zaidi na yenye ufanisi katika kujikusanyia alama nyingi muhimu. Majaji wawili walimpa Ugas alama 116 kwa 112 za Pacquiao, na Jaji wa tatu alitoa alama 115 kwa Ugas, na 113 kwa Pacquiao.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com