=============
Zanzibar, 18 Agosti 2021 – Katika muendelezo wa kuhamasisha shughuli za maendeleo pamoja na utamaduni, sanaa na michezo ili kuwaleta pamoja wakazi wa eneo la Kizimkazi visiwani Zanzibar, Benki ya CRDB imeandaa tamasha la Kizimkazi ambalo litafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 28 mwezi huu. Tamasha hilo la kila mwaka lililoanzishwa mwaka 2016 linatarajiwa kuwa la kipekee kwa mwaka huu kutokana na kupewa nguvu kubwa na Benki ya CRDB.
Akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya CRDB, TullyEsther Mwambapa amesema kuwa Lengo la CRDB Bank ni kulifanya tamasha hili kuwa endelevu, lenye kutangaza vivutio mbalimbali vya Zanzibar, kuchochea utunzaji wa mazingira and kutoa fursa za kiuchumi kwa wana Kizimkazi. Kizimkazi ina utajiri mkubwa wa vivutio vya kiutalii ikiwemo fukwe, dolphins, hoteli za Kisasa, tamaduni na historia ya Kizimkazi. Kupitia matangazo yetu mbalimbali mtaona na kusikia hazina kubwa iliyoko Kizimkazi.
“Kwa mlichokifanya leo kwa waheshimiwa wabunge pamoja na wadau wenu wengine wa hapa Dodoma inadhihirisha ni kwa jinsi gani ambavyo Benki ya CRDB ipo karibu na jamii na hususan wadau wake lakini zaidi mlichofanya kwa wenye watoto wenye uhitaji ni kikubwa sana chenye kustahili pongezi na kuigwa na wengine ” alisema Mh. Tulia.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesisitiza kuwa benki hiyo inawachukulia wateja wake wote kama sehemu ya familia yake, hivyo Mwezi huu Mtakatifu unatoa fursa ya kushirikiana kuboresha mahusiano kwa kushiriki pamoja katika ibada ya funga na futari.
“Tunaendelea kutumia kipindi hiki pia kuonyesha shukrani zetu kwao kwa kuendelea kuichagua benki yetu; wakati huo huo tunaendelea kutekeleza wajibu wetu kwa jamii kwa kugusa makundi yenye mahitaji maalum,” alisisitiza Nsekela.
Nsekelea alisema mbali na kufuturisha wateja, Benki ya CRDB pia imekuwa ikitoa msaada wa futari kwa vituo vya kulelea watoto vyenye uhitaji mkubwa. Mwaka huu Benki ya CRDB imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia futari kwa vituo vya kulelea watoto 40 katika kanda zote nchini huku ikitarajia kufuturisha wadau wake wa Zanzibar mwishoni mwa wiki hii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay amewashukuru wateja wa Benki wakiwemo wabunge kwa kushiriki katika futari hiyo na kuendelea kuiunga mkono Benki na kuiwezesha kuendelea kufanya vizuri sokoni.
Futari hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai pamoja na mawaziri mbalimbali wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na Sheikh Mustafa Shaaban, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambae aliiongoza dua ya kuiombea Benki ya CRDB kwa kufuturisha katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Social Plugin