Aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2017/19, Samson Lutema Lutonja amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa jimbo la Ushetu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Agosti 30,2021 muda mfupi baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilayani Kahama Lutonja amesema amedhamiria kuwaunganisha wananchi wa jimbo Ushetu katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
“Nitaanzia pale alipoishia mtangulizi wetu aliyetangulia mbele za haki kama chama changu kikinipa ridhaa ya kugombea jimbo la Ushetu, Elias Kwandikwa alifanya mambo mengi katika jimbo hili,nitayaishi mazuri yake,”amesema Lutonja.
Amesema kuwa kupitia uzoefu alioupata ndani ya chama wakati akiongoza Cmoja wa vijana wilaya ya Kahama (UVCCM) utamsaidia kuongoza kwa weledi pindi atakapopata nafasi hiyo.
Social Plugin