Hii ni baada ya mahakama ya Uganda kushikilia uamuzi wa awali ukitaja kisa hicho kama wizi.
Kwa mujibu wa Daily Monitor, kesi hiyo ilisikizwa mara ya kwanza mjini Masaka na uamuzi ulitolewa na Jaji Margaret Oumo-Oguli mnamo Aprili 25, 2013.
Mahakama ilifahamishwa kuwa mnamo Mei 21, 2012, Kasasira aliingia katika duka linalomilikiwa na Bi. Nazziwa akinyonyesha na kuchukuwa sigara, mandazi, na USh 15,000 (KSh 460) pesa taslimu.
Nazziwa alishuhudia kuwa alitoka nje kuchunguza kilichokuwa kikiendelea baada ya kusikia sanduku lake la pesa likifunguliwa dukani.
"Wakati Kasasira alimuona Nazziwa, alichomoa kisu ndani ya suruali yake na kumuonyesha. Hata hivyo, mwathiriwa alikuwa jasiri na kumpokonya Kasasira kisu hicho," ilisoma ushuhuda wa Nazziwa.
Mtafaruku huo uliwavutia wapita njia ambao walikimbia kumuokoa Nazziwa na kupambana na mshtakiwa.
Kisu ambacho alijaribu kumtishia mama huyo, kilipatikana pamoja na maandazi saba, vijiti tisa vya sigara na pesa.
Akata rufaa
Licha ya kukiri makosa yake, Kasasira hakuridhishwa na uamuzi huo na kuamua kuwasilisha kesi ya rufaa katika Mahakama ya Rufaa akitaka kesi hiyo kusikizwa upya. Kulingana naye, jaji alifanya makosa kwa kumhukumu miaka 15 gerezani, ambapo si sawa kwani makosa yake yalikuwa madogo.
Rufaa hiyo ilisikwa na jopo oa majji watatu wab Majakama ya Rufaa, Stephen Musota, Cheborion Barishaki, na Muzamiru Mutangula Kibeedi. Baada ya kusikiza rufaa hiyo kwa makini, majaji hao waliamua kwa kauli moja kuwa mshtakiwa anastahili adhabu hiyo aliyopewa awali. "Hukumu ya Mahakama Kuu ya miaka 15 gerezani kwa kupatikana na hatia ya wizi kinyume cha kipengele cha 285 na 286(2) cha sheria inashikiliwa," ilisoma uamuzi huo.
Hukumu wa Kasasira ulisomwa bila yeye kuwepo kutokana na masharti ya COVID-19 huku akiwakilishwa na wakili wake Lawrence Yawe.
Social Plugin