Mkazi wa kata ya Malezi wilayani Handeni mkoani Tanga, Nassoro Mustapha anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali mwilini ikielezwa sababu ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo limetokea jana Agosti 3, 2021 katika mtaa wa Kwamaraho inadaiwa kuwa mwanaume huyo alikuwa na ugomvi na mkewe na ndio uliomrudisha nyumbani.
Dada wa marehemu, Rehema Hemed amesema wanahisi tukio hilo limetokana na wivu wa mapenzi kwa sababu wanandoa hao walikuwa na ugomvi na kwamba shemeji yake alikuja nyumba wakiwa hawapo na kumshambulia mdogo wake.
Rehema amesema ndugu yake amefariki akiwa ni ujauzito wa miezi sita au na ameacha mtoto wa miaka mitatu.
Social Plugin