Na Abel Paul Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Mary Kipesha amewaongoza Maofisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika kuuaga Mwili wa askari Miraji Isingay ambaye alifariki dunia wakati wa mapambano ya askari na Kijana mmoja aitwaye Hamza Mohamed huko Dar es salaam katika Ubalozi wa Ufaransa ambapo katika tukio hilo askari wanne waliuawa huku muuaji naye akiuawa.
Katika Misa iliyoongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Rothia Agustino kwenye mahubiri yake amesema "Sisi sote ni wapitaji yatupasa kujiandaa vyema tukiwa hapa duniani kwa kutenda wema na kumcha Mungu kama ....kijana huyu Miraji ambaye amelala kwa kutekeleza majukumu ya kulinda faia na mali zao".
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP MARY KIPESHA amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Samia Hassani Suluhu ametoa pole kwa wanafamilia kwa kumpoteza mpendwa wao ambaye amefariki dunia wakati akitekeleza majukumu yake
Pia amesema kuwa jambo ama tukio hilo limewapa ari na chachu zaidi ya kupambana na wahalifu ambao wana dhamira ya kuvuruga amani ya nchi akibainisha kuwa kamwe Jeshi la Polisi halito wafumbia macho watu wa aina hiyo.
Wakati huo ndugu wa marehemu pamoja na wanawakjiji wamelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa upendo wa pekee waliouonyesha katika kumsindikiza kijana wao kwenye makazi yake ya milele.