Usimamamizi wa Taasisi ya Kiufundi ya St. Bernadette mjini Novrongo katika eneo la kati mwa Ghana umesimamisha masomo ya wanafunzi wanne kwa muda baada ya wanafunzi hao kumuibia mwalimu mkuu wa shule yao kanga watano na mbuzi wawili.
Uhalifu huo uliwapelekea wanafunzi hao ambao walikuwa katika mwaka wao mwisho, kufukuzwa shuleni.
Kwa mujibu wa ripoti ya MyNewsGH, wanafunzi hao walinaswa baada ya msako kufanywa na kubainika kuwa tayari walikuwa wameandaa kitoweo cha wanyama hao.
Wanafunzi hao walikamatwa lakini baadaye waliachiliwa kwa dhamana
. Kila mwanafunzi aliagizwa alipe faini ya KSh 9,000 kugharamia ujinga wao.
Social Plugin