Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi akizungumza leo Mkoani Morogoro.
Na Jackline Lolah Minja - Morogoro
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi amekataa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Mazimbu iliyopo katika Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro baada ya kuwa na mkanganyiko wa nyaraka zinazohusu shule hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa majengo ya shule ya sekondari Mazimbu leo Jumatano Agosti 10,2021 Luteni Josephine Mwambashi amesema hakuna mchanganuo halisi wa fedha zilizotumika kujenga majengo ya madarasa hayo yenye thamani ya shilingi milioni 65.
Aidha kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru amemuagiza mkuu wa wilaya ya Morogoro ,Albert Msando kuhakikisha anafuatilia nyaraka zote za mradi huo.
Social Plugin