Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija
Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija amewaomba wananchi wa Halmashauri ya Jiji hilo kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru unaokuja kuzindua miradi mbalimbali uliobeba dhima ya Uhuru na Umoja
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza la Madiwani amesema Mwege huo wa Uhuru utakimbizwa Tarehe 18 Agosti, 2021 na unatarajiwa kuzindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa, na moja kati ya miradi itakayotembelewa ni 'Kituo cha Mapato cha Buguruni' na kuonesha Wilaya ya Ilala inavyotumia kwa usahihi TEHAMA kuwahudumia Wananchi ipasavyo chini ya kaulimbiu ya Mwenge isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu. Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”.
Sanjari na hayo amesema Mwenge huo utakimbizwa katika miradi hiyo baada ya hapo utaenda kukesha katika shule ya Msingi Kiwalani wananchi watapata viburudisho mbalimbali ikiwemo muziki na ulinzi mkaliutaimarishwa siku hiyo
"Karibu Mwenge Maalum wa Uhuru Wilaya ya Ilala, Wilaya iliyobeba sehemu kubwa ya Historia ya Mkoa wa Dar es Salaam, kwa maana ya vivutio na uzuri unaolifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji 10 yenye mvuto zaidi Barani Afrika, vivutio vilivyopo Ilala ni kama vile; Sanamu ya Askari, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Ikulu ya DSM, Ukumbi wa Karimjee, Bandari ya DSM, Soko la Kariakoo, Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja, Kituo cha Reli ya DSM, Hospitali ya Muhimbili, Mnara wa Saa, Hoteli zenye hadhi ya Kimataifa, Soko la Samaki Feri, Benki Kuu ya Tanzania, Boma la Kale, Sekondari ya Pugu, Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere",alisema Ludigija
Pamoja na vivutio vyote hivyo kuwepo Wilaya ya Ilala, lakini pia shughuli mbalimbali za kibiashara hufanyika kwenye Wilaya hii inayoongozwa na Mhe. Ludigija, hivyo Ilala imeitambulisha Dar es salaam kuwa Jiji mashuhuri kwa biashara.
Social Plugin