Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI DAR WAANIKA MAJINA YA WALIOSAMBAZA VIDEO ZA UTUPU MTANDAONI


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne
 **
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili waliokuwa faragha na kisha kuzisambaza mitandaoni kwa madai ya kwamba wamewafumania.

Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, alilolitoa Agosti 6, 2021, Jijini Dar es Salaam, baada ya kuona video inayosambaa mitandaoni ikionesha mwanamke na mwanaume waliokuwa faragha wakidhalilishwa kwa kupigwa wakiwa watupu.

Taarifa ya kukamatwa kwao imetolewa na Kamanda wa Kanda hiyo Muliro Jumanne, ambapo ameyataja majina ya waliokamatwa kuwa ni Singiba Buchadi, Dephina Buchadi, Doratea Mathayo, Wilbard Teobardi, Albert Buchadi na Valenzi Silvester ambao wote ni wakazi wa Kongowe, na kwamba ukatili walioufanya ni wakutoa adhabu ilhali wao si Mahakimu wala Majaji.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com