Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye moja ya vikao vya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga .Kushoto ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
****
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Mathew Nkulila (57) ambaye ni Diwani kata ya Ndembezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 23,2021 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yanamsumbua.
Kufuatia msiba huu ambao umegusa watu wengi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi ameandika ujumbe ufuatao.
"Mungu wangu, ni sikitiko na hakika ni pigo kubwa kwa Manispaa ya Shinyanga, Wananchi na Mkoa kwa ujumla. Alikuwa mtu mwenye msimamo thabiti usioyumba kwa jambo aliloliamini.
Aliyapokea maono ya kuipelekea Shy MC kuwaJiji tangu tulipoandaa Mkakati wa Maendeleo wa Shinyanga 2018 kwa kuweka maono yetu.
Tulijipanga vema kuboresha huduma ya usafiri wa umma kwa kuanzisha daladala za Hiace kwa awamu 3 katika route 9 zilizobuniwa, kuanza kwa maonesho ya aina 4, kwa kuanza na ya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini, yangefuata ya taasisi za Fedha (Financial Institution Exposition), Afya (Health services Tech Exh) na Elimu (Education Exhibition).
Aliyapokea maono ya kuanzisha Shinyanga Olympic eneo la Kizumbi. Alipokea maono na tulishapanga na kuteua maeneo 7 ya kujenga vyuo vikuu na vyuo vya kawaida. Upimaji wa haraka kule Mwawaza na Galamba kwa vyuo vikuu 2 na kimoja cha chama.
Mkakati wa eneo la Tanganyika Packers kuwa eneo la Uwekezaji wa Viwanda (industrial park), kuitisha mkutano wa Wawekezaji ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa Wafanyabiashara kwa ajili masoko ya nazao na kuifanya Shy MC kuwa really logistic centre na mengine mengi ya viwanda na huduma kupitia mikopo ya wanawake na vijana ambapo zaidi ya bilioni 1.2 tulishatoa
Ooh rafiki yangu Mh Nkulila nimesikitika sana, nilimwelewa na alinielewa na hatimaye tukaelewana. Alikuwa ana uwezo wa kusukuma jambo likafanikiwa. Mungu ni mwema.
Hakika ninawapa pole sana Wanafamilia, Mkurugenzi, Wah Madiwani, Watumishi wa Shy MC, CCM, viongozi ofisi ya RC na DC na Wananchi kwa ujumla.
Naam, uongozi upo, Kamati ya fedha na Mkurugenzi wapo imara kutimiza matumaini ya Wananchi. LHSRIP
Social Plugin