Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba amefariki duniani Agosti 3, 2021 majira ya saa 1 jioni katika hospitali ya Rabinitsia iliyopo jijini Dar es salaam aliyokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Askofu wa jimbo katoliki Kigoma, Evarist Guzuye, amesema misa takatifu ya mazishi itafanyika katika kanisa la Mtakatifu Marko Kabanga, wilayani Kasulu siku ya Jumatatu, Agosti 9, 2021.
Social Plugin