Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa uliyopo Kata ya Bonyokwa jijini la Dar es Salaam, Shabaan Maliyatabu
Na Fatma Ally - Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa uliyopo Kata ya Bonyokwa jijini la Dar es Salaam, Shabaan Maliyatabu awewataka wanawake wa Kata hiyo kuwa na matumizi mazuri na pesa wanazipata hasa wanazokwenda kukopa kwenye Taasisi mbalimbali.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la Wanawake piga kazi lililoandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mtaa kwa kushirikiana na Shirika la haki za wanawake (HAWA) chini Mkurugenzi wake Joyce Kiria.
Amesema kuwa, kongamano hilo limelenga kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwakutanisha pamoja ili waweze kujifunza kupitia watu waliofanikiwa na kupata fursa mbalimbali za biashara.
Ameeleza kuwa, asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kuchukua mikopo bila kujua wanakwenda kufanyia nini, ambapo wengine huanzishia biashara jambo ambalo hupelekea watu wengi kushindwa kulipa deni.
"Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa tumejipanga kuwaenua wanawake wa Bonyokwa waondokane na kuwa tegemezi, tutaandaa hii siku maalum kwa ajili yao (wajasiriamali day) tutawakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ambao watakuja kutoa elimu lengo ni kuwawezesha kiuchumi",amesema Maliyatabu.
Aidha, amewataka wanawake hao kujiunga vikundi kuanzia watu watano, kufuata tararibu zote na kwenda Halmashaur kwa ajili ya kupata mkopo wa asilimia 10 ambao hauna riba, ambao umehusisha kila idara, ikiwepo 6 asilimia 3 vijana, 3 wanawake, 2 walemavu na 2 akina baba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la haki za wanawake (HAWA) Joyce Kiria amewataka wanawake hao kuhudhuria makongamano mbalimbali yanayoandaliwa ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa, wanawake wanatakiwa wabadilike Ulimwengu wa sasa hivi upo kiganjani, hata kama wapo nyumbani lakini watafute kitu cha kufanya na kuuza mtandaoni waachane na maisha ya kuwa tegemezi.
"Wanawake munatakiwa kujitambua na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kuweza kujipatia kipato, tumia bando lako ili uweze kuleta mabadiliko katika jamii yako, jifunze kwa waliofanikiwa usichoke",amesema Kiria.
Kongamano hilo limewashirikisha wadau mbalimbali kutoka Shirika la haki za wanawake (HAWA) ikiwemo wanasheria, Afisa miradi pamoja na wadau wa maendeleo na wajasiriamali.
Social Plugin