WATENDAJI WA SHIRIKA LA POSTA WAFUNDWA KUENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA DUNIANI


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew

Na Magrethy Katengu - Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amewataka viongozi wa shirika la Posta nchini kuenda na kasi ya mabadiliko ya Tehama duniani kwa kuziweka tayari fikra zao kujifunza mara kwa mara.

Wito huo ameutoa jijini Dar es salaam wakati akifunga kikao kazi cha mameneja wa mikoa kilichoadhimia kuboresha ufanisi wa utendaji kazi wao ambapo amesema kiongozi bora ni yule anayeweza kuyageuza maono kuwa katika uhalisia.

"Itanishangaza Kauli mbiu Yenu Mkisema Posta Kiganjani Twende Kidigitali halafu cha Kushangaza Mtendaji wa Posta anatoa huduma kwa wateja kupitia simu ya Kitochi, nakuagiza Kaimu Posta Masta uangalie hiyo kwa makini",alisema Naibu Waziri

Aidha mhandisi Kundo amemtaka kaimu Poster Master Mkuu kuwawezesha mameneja wa mikoa kwa kuwapatia vifaa vya kazi ikiwemo magari na vishikwambi vitakavyowafanya kuenda na msemo wa posta kidigitali zaidi.

Kwa upande wake kaimu posta master mkuu  Macrice Mbodo alisema kupitia kikao kazi hicho wameweza kupitia mambo 12 ikiwemo kupata mafunzo ya uongozi,mfumo wa serikali mtandao,kupitia mifumo ya posta kidigital ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya utenda wa shirika kwa mwaka 2020/2021.

Sanjari na hayo mameneja wa mikoa wa posta wamesaini mikataba ya makubaliano ya kiutendaji inayolenga kuchochea kasi ya utendaji kazi na ubunifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم