MABINTI WA RAFIKI SDO WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA..WAONESHA BIDHAA ZAO

Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) na Mabinti wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki SDO limeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyofungwa leo  Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kwa kuonesha na kuuza bidhaa zinazotengenezwa na Mabinti wanaofadhiliwa na shirika hilo kwa lengo kuwainua kiuchumi.

Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage amesema wanawasaidia mabinti kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu za ujasiriamali, akiba na uchumi ambayo inawawezesha kupitia hizo akiba kupata mikopo katika vikundi vyao kuanzisha biashara zao binafsi na kuwafanya wasiwe wategemezi na kuwaepusha na vishawishi na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mabinti kutoka Rafiki SDO wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) akiwa banda la Rafiki SDO kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.

Wananchi wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na mabinti katika banda la Rafiki SDO kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akimkabidhi Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO Ahsante Nselu (kulia) cheti cha Mshindi wa pili kwa NGO's kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post