Wanasayansi wamezidi kushangazwa na kilichosababisha mtoto mmoja wa kiume aliyezaliwa na sehemu tatu za uume nchini Iraq miezi kadhaa baada ya kumfanyia oparesheni ya kuondoa sehemu mbili .
Tukio hilo watalaam wanasema ndilo lilikuwa la kwanza kwa binadamu kuzaliwa na sehemu tatu za siri katika kinachojulikana kitaalam kama triphallia. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na sehemu tatu za uume katika eneo la Duhok nchini Iraq na mara ya kwanza madaktari walimuona akiwa na miezi mitatu .
Tangia hapo wamekuwa wakiendelea na utafiti wa kung'amua kwanini alizaliwa na sehemu hizo tatu lakini hadi sasa hawajapata majibu .
Alifanyiwa upasuaji kuondoa sehemu mbili kati ya hizo tatu ambazo zilikuwa zimeanza kujitokeza katika shina la eneo la korodani .Sehemu ya tatu ilikuwa katika eneo la kawaida ambapo uume wa mwanamme huwa .
Kulingana na uchunguzi wa kisa hicho uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Upasuaji la Novemba mwaka jana , kijana huyo alikuwa akiendelea vizuri katika ziara ya ufuatiliaji mwaka mmoja baada ya upasuaji.
Uume wa ziada, au "usio wa kawaida" ni hali nadra ya kuzaliwa, inayotokea mara moja tu katika kila watoto milioni 5 hadi milioni 6 wanaozaliwa kulingana na watafiti.
Sehemu mbili kuondolewa
Kiwango cha ukuaji wa sehemu hizo kwa jina la kitalaam -phallus hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine
Katika tukio la mtoto huyo wa Iraq, sehemu hizo mbili za ziada zilikuwa na tishu za erectile, ziitwayo corpus cavernosum, ambazo hujaa damu wakati wa kuamka, na vile vile tishu inayoitwa corpus spongiosum, ambayo inasaidia mrija unaotumiwa kupitisha mkojo.
Lakini sehemu hizo za uume wa ziada hazikuwa na mirija ya kupitisha mkojo yaani urethra . Hii ilifanya kuondolewa kwa upasuaji kwa viungo hivyo vya ziada kuwa rahisi.
Haijulikani sana juu ya kwanini uume wa ziada huibuka, alisema John Martin, profesa wa anatomia katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha St. Louis
Martin na wenzake wanaofundisha anatomia kwa kutumia mpango wa kuchangia sehemu za miili ya watu wakati mmoja waligundua kuwa mmoja wa wafadhili wa mwili wao alikuwa na diphallia, au sehemu mbili za uume. Mwanamume huyo, ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 84, alikuwa na sehemu mbili za siri zenye ukubwa kamili na pengo la urethra kati yazo katika shina la korodani
Mfadhili hakutaja hali yoyote kwenye fomu zake za kuchangia mwili. Alikuwa na watoto wawili, Martin alisema, lakini watafiti hawajui ikiwa walikuwa watoto wake kibaolojia au ikiwa teknolojia yoyote ya uzazi ilikuwa muhimu kwa mwanamume huyo kupata watoto.
Via Mwananchi
Social Plugin