Mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa mmoja wa wamiliki wa mabasi ya Sumry, Humud Sumry, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatatu Agosti 09, 2021 jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika na anatarajiwa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.
Enzi za uhai wake, Sumry aliyekuwa na makazi yake, Nkasi mkoani Rukwa alikuwa akifanya biashara ya usafirishaji wa abiria kupitia mabasi ya Sumry na baadaye, aliamua kuachana na biashara hiyo na kuwekeza katika kilimo.
Social Plugin