Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson David Msumba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendji wa Halmashauri za Jiji, Miji, Manispaa na Wilaya ambapo kwa upande wa Mkoa wa Shinyanga amemteua Nice Remen Munissy kuwa Mkurugenzi wa wilaya ya Shinyanga, Charles Edward Fussi wilaya ya Msalala akichukua nafasi ya Simon Berege aliyepelekwa wilaya ya Maswa, Lino Pius Mwageni wilaya ya Ushetu akichukua nafasi ya Michael Augustino Matomora aliyepelekwa wilaya ya Iramba, Jomary Mkristo Satura Manispaa ya Shinyanga huku akimbakiza Emmanuel Johnson Matinyi katika wilaya ya Kishapu na Anderson Msumba katika Manispaa ya Kahama.
Social Plugin