Waziri wa Maliasili na Utalii Damas Ndumbaro
Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Damas Ndumbaro ameitaka Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) kuwanyang'anya ndani ya siku 60 Wawekezaji wa Vitalu vya Wanyamapori ambao wameshindwa Kupambana na Majangili na kuzuia na uingizwaji wa mifugo katika maeneo yao.
Amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini Cheti na kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Bushman Hunting Safari's Talala Abood ambapo amesema hiyo ni kampuni ya kwanza ya Mzawa kuwekeza hapa nchini hivyo itakuwa chachu kwa Wawekezaji wengine kujitokeza ndani na nje ya nchi
"Niseme hii ni kampuni iliyofanikiwa kupata Cheti kwani kulikuwa kampuni 10 zilizoiingia katika mchakato wa kutuma maombi na leo wanakabidhiwa Cheti Cha kuendelea na shughuli za kuwekeza", alisema Ndumbaro.
Hata hivyo amesema Wawekezaji wanaohitaji kuwekeza katika Vitalu wa ndani wawe na kiasi cha Fedha cha dola milioni 10 huku mwekezaji kutoka nje ya Nchi ni kiasi cha Fedha dola milioni 150.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) Meja Generali Mstaafu Hamis Semfuko amesema mchakato wa shughuli hiyo ya kusainiana vyeti ilianza mwaka 2018 itakuwa ni chachu kwa Makampuni mengine yaliyokatika mchakato kama huo kuja kuwekeza ili kusaidi kuongezeka pato la Taifa.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Bushman Hunting Safari's LTD Talala amesema anaishukuru TAWA siku hii ya leo ambayo imekuwa ya pekee kwani kwa fursa pekee waliyoipata watajitahidi kuendeleza maeneo yaliyowazi ambapo wataendeleza ushirikiano kati yao na Serikali kwa kuhakikisha kunakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
Social Plugin