Na Jackline Lolah Minja - Morogoro
Kuelekea siku ya Wananchi itakayofanyika Agosti 29 ,2021 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam , viongozi na mashabiki wa Yanga SC mkoani Morogoro wameiadhimisha kwa kushiriki usafi katika maeneo mbalimnali ikiwemo Stendi ya Mabasi ya Msamvu, eneo la Makaburi ya Wahanga wa moto na kutembelea watoto yatima katika kituo cha Mihayo kilichopo Mazimbu mkoani Morogoro.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya viongozi pamoja na mashabiki wa timu hiyo wakiongozwa na Mhandisi Bahati Mwaseba ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga wameomba wapenzi na wadau wa mpira kuhudhuria siku hiyo ili kuendelea kuleta hamasa ndani ya klabu hiyo.
Social Plugin