Mkazi wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu mkoani Manyara, Harold Hhando anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Emmanuela Hhando (13) na kumtoa viungo vya mwili.
Inadaiwa Hhando alimuua mtoto huyo kwa kumpasua katikati ya miguu na kumtenganisha vipande viwili kisha kukata sehemu za siri, kumtoa maini na kutaka kuyapika ili ayale.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo lilitokea jana kijijini hapo.
Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha tukio hilo ni ushirikina kwani Hhando ameeleza kuwa aliambiwa na mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi.
Chanzo - Mwananchi
Social Plugin