Na Magreth Katengu - Dar es salaam
Tanzania inaendelea kupiga hatua kiuchumi na kiteknolojia hivyo Taasisi za fedha hazina budi kuwasogezea wananchi huduma hizo karibu kwa njia ya kidigital ili kuwasaidia kuokoa muda wanaotumia kutembea mwendo mrefu kufuata huduma.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Akiba Bank Dora Saria jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa huduma ya wakala ijulikanayo kwa jina la Akiba Wakala ambapo amesema huduma hiyo itawasaidia wateja kupata huduma kwa urahisi popote pale walipo kupitia mtandao
Amesema benki hiyo imekuwa mshiriki mzuri katika kuunga mkono harakati za serikali za kuhakikisha uwepo wa huduma jumuishi za kifedha kwa watanzania wote
"Tumeingia sokoni na jumla ya wakala wapatao 200 na tunaendelea kukidhi kiu ya upatikanaji wa huduma kufuata mteja potote alipo kwa kumpatia huduma zetu ikiwemo Amana,mikopo,kutoa na kuweka fedha", alisema Dora
Kwa upande mmoja wa wakala wa ACB Faidha kiiwiri amesema mchakato wa kutumia huduma ya benki hiyo gharama zake utoaji pesa kupitia wakala gharama zake ni nafuu zaidi kupitia kazi hiyo kama kijana amejiajiri na maisha yake yamebadilika
Aidha amewaomba watu wote wajiunge na benki hiyo kwani imekuwa mstari wa mbele kusaidia na kuwainua watu wenye kipato cha chini kwa kuwakopesha kwa riba nafuu ili wainue uchumi wao
Social Plugin