Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Family Health International (FHI 360) limetoa msaada wa Baiskeli 242 kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Hafla fupi ya makabidhiano ya Baiskeli hizo imefanyika leo Jumatatu Agosti 16,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.
Akipokea baiskeli hizo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amelipongeza Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC, wafadhili wa mradi USAID na PEPFAR pamoja na asasi za kiraia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia na kusaidiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa makundi yaliyoko kwenye athari za kupata maambukizi ya VVU hasa mabinti.
“Wawezeshaji kiuchumi nendeni mkafanye kazi kwa niaba ya serikali. Kafanyeni kazi ya kuwafikia mabinti ili tupunguze maambukizi ya VVU katika jamii yetu,toeni elimu ya miundo na uchumi ili wasichana wafanye kazi na kupata mitaji na kupunguza tabia hatarishi za kupata maambukizi ya VVU”,amesema Dkt. Sengati.
Amesema kwa mujibu wa Tanzania HIV Impact Survey ,2016-17, takwimu zinaonesha hali ya maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na wamama vijana ni asilimia 15.3% ukilinganisha na umri wao huo ambao ni asilimia 6.6%.
“Pia kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania na Utafiti wa Kiashiria cha Malaria, 2015 - 16 takwimu zinaonesha asilimia 27 ya wasichana balehe wenye umri wa miaka kati ya 15-19 wamepata mtoto au ujauzito”,ameeleza.
“Kutokana na takwimu hizo inaonesha ni jinsi gani wasichana balehe na wamama vijana wako katika athari kubwa na wanapaswa kulindwa na kuhakikisha tunapunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI miongoni mwao”,ameongeza Dkt. Sengati.
Mkuu huyo wa mkoa ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha yanaifikia jamii na kutoa eleimu ya kutosha ili kupunguza changamoto zinazowakumba wasichana zikiwemo mimba za utotoni,ukatili wa kijinsia na maambukizi ya VVU na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuwa na jamii inayomthamini mtoto wa kike na kumpa ulinzi wa kutosha.
“Serikai tunatambua na kuthamini mchango wa wadau na hatuwezi kufanya kila kitu ndiyo maana nyinyi kama wadau mko mstari wa mbele kuisaidia serikali kutekeleza agenda ya maendeleo ya 2030 na kuhakikisha kwamba 95-95-95 (95 % ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali yao ya maambukizi, 95% ya waliopima wameanza kutumia dawa na 95% ya walioanza dawa wamepunguza makali ya VVU”, amesema Dkt. Sengati.
Akikabidhi baiskeli 24 kati ya 242 Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka amesema Shirika la Family Health International (FHI 360) limetoa baiskeli hizo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kimataifa wa EPIC kwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
“Kupitia mradi huu tumetoa jumla ya baiskeli 242 kwa mkoa wa Shinyanga ambazo zinagawiwa kwa walengwa katika halmashauri 5 za wilaya ambazo ni Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kahama, Ushetu na Msalala. Leo tumekusanyika hapa kwa dhumuni la kugawa baiskeli kwa wawezeshaji uchumi 24 wa Manispaa ya Shinyanga”,amesema Dkt. Msuka.
Ameeleza kuwa baiskeli hizo zitasaidia Wawezeshaji Kiuchumi kuwafikia wa wasichana balehe na wamama vijana na kuchangia jitihada za serikali katika kuhakikisha maambukizi ya VVU/UKIMWI yanapunguzwa na kufikia malengo ya 95-95-95.
“Baiskeli hizi ni sehemu ya vitendea kazi kwa wawezeshaji uchumi,tunaamini zitapunguza changamoto ya usafiri na kuwawezesha kuwafikia wasichana wengi zaidi katika kata, vijiji,vitongoji na hata ngazi ya kaya”,amesema Dkt. Msuka.
“Baiskeli hizi zinapaswa kutumika kwa matumizi ya mradi tu na si vinginevyo ili kuboresha hali ya mabinti na kutokomeza janga la UKIMWI. Tanzania bila UKIMWI inawezekana, tuendelee kutoa elimu kwa kila mtu asimame katika nafasi yake kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI nchini Tanzani”,ameongeza Dkt. Msuka.
Dkt. Msuka amesema Mradi wa EPIC unatekeleza afua za utoaji wa huduma zinazohusiana na VVU zikiwalenga makundi maalumu na yanayohitaji kupewa kipaumbele ikiwemo wasichana wa rika balehe na wamama vijana, wanaume na wanawake walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.
Amefafanua kuwa Mpango wa DREAMS ni kati ya afua zinazotekelezwa na mradi wa EPIC wenye lengo la kupunguza maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka 9 hadi 24, wanaoishi katika mazingira hatarishi na wanafanya ngono katika umri mdogo ili waweze kumudu gharama za maisha.
“Mradi wa EPIC unatekeleza mpango wa DREAMS katika halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga tangu mwezi Februari 2020 kupitia mashirika manne ya kijamii ambayo ni Rafiki SDO, TADEPA, HUHESO Foundation na SHIDEPHA. Tayari jumla ya wasichana 100,000 wamefikiwa.
“Wasichana 20,000 wamefikiwa na huduma za kitabibu kama upimaji wa VVU kwa hiari,uchunguzi wa ukatili wa kijinsia,huduma za uzazi wa mpango,uchunguzi wa magonjwa ya zinaa na huduma za dawa kinga (PREP), 38,000 wamefikiwa na huduma za miundo ambako wanaweka akiba na kukopa, 13,000 wameweza kuanzisha biashara zao wenyewe na 100,000 wamefikiwa na huduma za mabadiliko ya tabia”,ameongeza.
Akizungumza kwa niaba ya Wawezeshaji Uchumi,Sophia Chamba amelishukuru Shirika la FHI 360 na Mradi wa EPIC kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia kuifikia jamii kutekeleza majukumu yao ambayo ni pamoja na kuwafundisha mabinti balehe na wanawake vijana masomo ya uchumi na yanayosaidia kujikinga na maambukizi mapya ya VVU.
Ameyataja majukumu mengine kuwa ni kutoa elimua ya mabadiliko ya tabia na upimaji wa VVU kwa kushirikiana na waelimisha rika,kufundisha masuala ya ujasiriamali na kuandikisha mabinti balehe na wanawake vijana katika vikundi kulinga na umri wao.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akikabidhi baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mwezeshaji Uchumi,Sophia Chamba akilishukuru Shirika la FHI 360 na Mradi wa EPIC kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia kuifikia jamii kutekeleza majukumu yao.
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Shinyanga Geofrey Mambo akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikagua baiskeli moja kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiendesha baiskeli ambayo kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Rachel Manga (kulia). Kushoto ni Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Amina Bundala (kulia). Kushoto ni Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Elizabeth Sollo (kulia). Kushoto ni Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Mary Ford (kulia). Kushoto ni Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakiendesha baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhiwa baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin