Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed (kushoto) akikabidhi sehemu ya Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul (kulia) kwa ajili ya wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Bima la Taifa ( National Insurance Corporation –NIC) limetoa msaada wa Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti Angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Akizungumza leo Jumatano Agosti 25,2021 wakati wa kukabidhi Vibao na Vesti Angavu hizo kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul, Meneja wa NIC Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed amesema vitasaidia kuzuia ajali za barabarani.
“Tumekabidhi vibao na Vesti angavu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 ili visaidie kuzuia ajali za barabarani mkoani Shinyanga ambapo viongozi wa wanafunzi watavaa Reflectors na watasimama kwenye kivuko ‘Zebra’ na kuonesha Vibao vyenye Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ ili kuruhusu wanafunzi wenzao kuvuka barabara au kutovuka”,amesema Mohamed.
Akipokea vifaa hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Joseph Paul ameishukuru NIC kwa msaada huo ambao utasaidia kuzuia ajali za barabarani kwa wanafunzi huku akibainisha kuwa watatumia vibao na vesti angavu walizopewa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SP Malege Kilakala amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kufundishia elimu ya usalama barabarani katika kuhakikisha wanafunzi wa rika zote wanavuka barabara salama.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji amesema NIC imefanya jambo jema kutoa vifaa hivyo akibainisha kuwa huo ni mwendelezo wa utoaji elimu ya usalama barabarani.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed (kushoto) akikabidhi sehemu ya Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul (kulia) kwa ajili ya wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni katika ukumbi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 23,2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed (kushoto) akimkabidhi Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul (wa pili kulia) Kibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ ambacho ni sehemu ya vibao 150 kwa ajili ya wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SP Malege Kilakala, wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed (wa pili kushoto) akikabidhi Viaksi Mwanga kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul (kulia). Vesti angavu hizo ni sehemu ya viaksi mwanga 100 vilivyotolewa na NIC kwa ajili ya wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SP Malege Kilakala, wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Emmanuel Pallangyo.
Muonekano wa sehemu ya Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti Angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 vilivyotolewa na NIC ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Muonekano wa sehemu ya Vesti angavu (Reflectors) 100 zilizotolewa na NIC ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed akizungumza wakati akikabidhi Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul akizungumza wakati akipokea Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 vilivyotolewa na NIC ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SP Malege Kilakala akizungumza wakati wa makabidhiano ya Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 vilivyotolewa na NIC ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akizungumza wakati wa makabidhiano ya Vibao 150 vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ na Vesti angavu (Reflectors) 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5 vilivyotolewa na NIC ili kusaidia wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.
Wafanyakazi wa NIC wakionesha Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Emmanuel Pallangyo akitoa elimu ya matumizi Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Mjini Shinyanga.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge Mika Paul Kekema akionesha vibao vinavyoonesha Ishara ya 'GO' na 'STOP' akiwa na wanafunzi wake waliovaa Vesti angavu viwasaidie wakati wa kuvuka barabara
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge Mika Paul Kekema akilishukuru Shirika la Bima la Taifa kwa kuwapatia vibao vinavyoonesha Ishara ya 'GO' na 'STOP' na Vesti angavu kwa ajili ya wanafunzi kutumia wakati wa kuvuka barabara
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Emmanuel Pallangyo akitoa elimu ya matumizi Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’ kwa vitendo barabarani kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Mjini Shinyanga.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwenge iliyopo Mjini Shinyanga wakijifunza kwa vitendo barabarani matumizi ya Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwenge iliyopo Mjini Shinyanga wakijifunza kwa vitendo barabarani matumizi ya Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin