Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Mwanahamisi Iddi (katikati) akimkabidhi Vifaa vya Marathon 'CRDB Bank International Marathon Kit', Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye pia ni Balozi wa Huduma ya SimBanking Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika leo Jumatano Agosti 18,2021 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. Kadama Malunde kutoka Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi waliojitokeza kushiriki na kusambaza tabasamu kupitia Mbio za CRDB Bank International Marathon 2021 zikizongozwa na Kauli mbiu 'Kasi Isambazayo Tabasamu' ambazo zimeendelea kutambulika kimataifa baada ya kupatiwa ithibati na World Athletics na AMIS na kwa sasa zina hadhi sawa na zile mbio za Boston Marathon za nchini Marekani.
Mbio za hisani za kimataifa zilizoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank International Marathon” kwa mwaka 2021 zimefanikiwa kuandika rekodi kwa kuvutia washiriki zaidi ya 5,000 ikiwemo maelfu ya raia wa kigeni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio hizo.
Jumla ya Shilingi za Kitanzania Shilingi milioni 500 zimefanikiwa kukusanywa ambazo zitaelekezwa kwa ajili ya kusaidia jamii.
Kati ya fedha zote Shilingi Milioni 500 zilizopatikana, Shilingi Milioni 200 zimeelekezwa watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo JKCI, Sh104 milioni zimeenda kujenga kituo cha mawasiliano cha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kiasi kilichobaki kimeelekezwa katika utunzaji mazingira kupitia kampeni ya Pendezesha Tanzania.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Mwanahamisi Iddi (katikati) akimkabidhi Vifaa vya Marathon 'CRDB Bank Marathon Kit', Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye pia ni Balozi wa Huduma ya SimBanking Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi. Kulia ni Afisa wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Godfrey Kidubo #CRDBBankMarathon2021 #kasiisambazayotabasamu
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye pia ni Balozi wa Huduma ya SimBanking Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Vifaa vya Marathon 'CRDB Bank Marathon Kit'.
Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akimkabidhi Vifaa vya Marathon 'CRDB Bank Marathon Kit' Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Bi. Ansila Benedict kutoka mkoa wa Shinyanga ambaye ni miongoni mwa maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi waliojitokeza kushiriki na kusambaza tabasamu kupitia Mbio za CRDB Bank International Marathon 2021 zikizongozwa na Kauli mbiu 'Kasi Isambazayo Tabasamu'.
#CRDBBankMarathon2021 #kasiisambazayotabasamu
Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akimkabidhi Vifaa vya Marathon 'CRDB Bank Marathon Kit' Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia Bi. Ansila Benedict kutoka mkoa wa Shinyanga ambaye ni miongoni mwa maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi waliojitokeza kushiriki na kusambaza tabasamu kupitia Mbio za CRDB Bank International Marathon 2021 zikizongozwa na Kauli mbiu 'Kasi Isambazayo Tabasamu'. #CRDBBankMarathon2021 #kasiisambazayotabasamu
Soma pia :
Social Plugin