CHANJO YA UKIMWI YAANZA KUFANYIWA MAJARIBIO KWA BINADAMU


HATIMAYE chanjo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya nchini Marekani inatarajiwa kuanza majaribio kwa binadamu kesho Alhamisi, Agosti 19, 2021.

Hatua hii imekuja baada ya kampuni hiyo ambayo inatengeneza chanjo za aina mbili za Ukimwi, kufuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu.

Chanjo hizo ni pamoja na mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core, ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa binadamu kwa mara ya kwanza. Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu 56 wa miaka 18-56 na majaribio yanatarajiwa kukamilika 2023.

Virusi vya Ukimwi viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1983-84 ambapo tangu miaka hiyo mamilioni ya watu wamepoteza maisha yao kutokana na janga hilo lisilo na kinga wala tiba. Moderna pia inatengenza chanjo ya mafua (influenza vaccine) kwa kutumia teknolojia hiyo hiyo iliyotumika kwenye virusi vya Ukimwi. Mpaka sasa Kirusi cha Ukimwi kimejibadili mara 16.

Moderna tayari wameshafanya majaribio ya kwanza (Phase I) ya chanjo ya VVU mwanzoni mwa mwaka huu ambayo iliangazia zaidi usalama wa chanjo hiyo kwa kuwanja watu waliojitolea wenyewe kwa hiari yao. Awamu ya pili (Phase II) itaangazia uthabiti (uwezo wake wa kufanya kazi kwa ujumla) na awamu ya tatu (Phase III) itaangazia iwapo chanjo hiyo inatosa majibu sahihi na yaliyokusudiwa pamoja na tiba.

Tofauti na chanjo za inactive au live, chanjo za mRNA haina sehemu ya mdudu (virus), badala yake imetengenezwa protein maalum ambayo huchochea kinga ya mwili, hivyo kuondoa baadhi ya madhara makubwa ambayo yangesababishwa na kumtumia kirusi cha Ukimwi kutengeneza chanjo hiyo pamoja na uhifadhi wa chanjo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم