Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt.Ellen Senkoro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Afya wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation Bw.Hendry Samke akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa huduma za afya Dkt.Isaac Maro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Taasisi ya Benjamini Mkapa leo Jijini Dar es Salaam
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano uliofanyika katika ofisi za Taasisi ya Benjamini Mkapa leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt.Ellen Senkoro akipata picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufanya mkutano leo katika ofisi za Taasisi za Benjamini Mkapa leo Jijini Dar es Salaam.
***********************
Serikali imejitahidi kuwekeza katika majengo ya huduma za afya hivyo kuna umuhimu wa kuwekeza pia katika rasilimali watu ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt.Ellen Senkoro katika ofisi za taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dkt.Senkoro amesema kuwa taasisi ya Benjamin Mkapa imekuwa ikijikita zaidi kuimarisha mifumo ya sekta ya afya ambapo wamegundua upungufu wa rasiliamali watu katika sekta hiyo.
"Hali halisi ya watumishi wa afya katika sekta ya afya bado ni changamoto,Tanzania tunahitaji kama watumishi laki mbili lakini mpaka sasa wapo asilimia 48% tu ambao ni takribani elfu tisini nane". Amesema Dkt.Senkoro.
Amesema wastani wa Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema angalau kuwe na daktari mmoja kati ya watu elfu moja lakini Tanzania ipo daktari mmoja kati ya watu elfu ishirini.
"Kuna utofauti mkubwa kati ya maeneo ya mjini na maeneo ya vijijini, kwa upande wa vijijini ni daktari mmoja kwa watu 78,000, wakati kwa mjini ni daktari mmoja kwa watu 9,000". Ameeleza Dkt.Senkoro.
Kwa upande wake Mtaalamu wa huduma za Afya Dkt.Issac Maro amesema uhitaji wa wahudumu wa afya katika vituo vya afya ni mkubwa hivyo kusababisha athari kubwa kutokea pindi mgonjwa akihitaji kujua afya yake.
"Kuwepo kwa upungufu wa wahudumu wa afya kumesababisha jamii nyingi kuishi na Virusi Vya Ukimwi bila kujua hivyo nimuhimu sana kuwepo kwa uwekezaji wa rasilimali watu kwenye vituo". Amesema
Hata hivyo amesema kuna maeneo mengine kuna majengo mengi ya kutoa huduma za afya pamoja na vifaa vya kutosha lakini hakuna wataalamu wa kuweza kutumia vifaa vya huduma za afya vilivyopo kwenye vituo vya afya.
Social Plugin