Dkt. Faustine Ndugulile
Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt. Faustine Ndugulile amesema takwimu za Matumizi rasmi ya mifumo ya fedha nchini bado sio nzuri ambapo asilimia 16.7% ya watu pekee ndio wanatumia huduma za benki,asilimia 48.6 wanatumia mitandao ya simu, asilimia 6.7 wanatumia njia zao binafsi na asilimia 28 hawatumi kabisa mifumo rasmi ya kifedha.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma za benki ya CRDB Ndani ya ofisi za Posta nchini ambapo amesema anawapongeza CRDB na shirika la posta kwa ushirikiano walionao ambao utasaidia kuwafikia watanzania asilimia 28 ambao hawatumia mifumo rasmi ya kifedha.
Aidha Wizara hiyo inaandaa mradi wa utoaji anuani za makazi kwa kutambua kila mtaa na nyumba kwa kodi maalumu jambo ambalo litasaidia shirika la posta na mengine kuwafikishia huduma, vifurushi na barua wananchi kwenye makazi yao.
Kwa upande Kaimu posta Master Mkuu Macrice Mbodo amesema serikali inaadhimia kutoa huduma zake ikiwemo huduma za RITHA,NIDA,TRA Na nyinginezo kupitia shirika la posta. Pia shirika limejikitaka katika utoaji wa huduma kidigital.
"Shirika la posta mpaka sasa lina ofisi zaidi ya 300 na kupitia kwa bia wake Dunia kote wana matawi zaidi ya laki sita", alisema Mbodo.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Abdulmakid Nsekela amesema takwimu zinaonyesha kuwa watu 10 sita kati yao wapo kwenye mifumo rasmi ya kifedha lakini wengi wanatumia mitandao ya simu ambapo katika baadhi ya huduma hushindwa kuzifanya ikiwemo kuhifadhi fedha nyingi kwa wakati mmoja.
Aidha amesema CRDB inaamimi katika ubunifu katika kutatua changamoto za wananchi na imejipanga kuwekeza zaidi katika mifumo ya tehama katika kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Social Plugin