Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LHRC YAIOMBA SERIKALI KUHIMIZA MAKAMPUNI,WAFANYABIASHARA KUFUATA HAKI ZA BINADAMU


Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga

Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kimeiomb serikali kuendelea kuhimiza wafanyabiashara, makampuni kufuata haki za binadamu mahali pa kazi na yeyote atakayekiuka sheria kali zichukuliwe ili kusaidia kuepuka vitendo viovu makazini ikiwemo rushwa,ubaguzi,unyanyaswaji hali utakayopelekea uchumi wa nchi kutopiga hatua kimaendeleo.

Ombi hilo limetolewa leo Jumanne Agosti 31,2021 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga katika ufunguzi wa Mdahalo na Sekta ya biashara ambapo amesema ni budi kampuni ijali mazingira ya Wafanyakazi wao kwani wengine hupitia changamoto ikiwemo kulipwa mshahara mdogo,kufanya kazi kwa muda mrefu, masaa 24 bila kupumzika hivyo kupelekea wengine kupata matatizo ya kiafya .

"Ni budi Makampuni kuhakikisha shughuli wanazizifanya kurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwetamo kununua vifaa mashuleni,hospitali kwani ujenzi wa Nchi lazima wahusike kwani nao hupata faida",alisema Anna Henga.

Kwa upande wake  Mshiriki katika Mdahalo huo Wilfred Mwakibala amesema Serikali haina budi kutengeneza sheria,taratibu zitakazosaisadia kulinda haki za binadamu zinalindwa mahali pa kazi

Hata hivyo ameongeza kwa kusema baadhi ya maeneo ya makazi wafanyakazi hawajaliwi na waliowaajiri kwani wanapopata ajili wawapo kazini kupatiwa matibabu ni changamoto kawa hawajakata bima wenyewe hivyo serikali haina budi kusimamia sheria za wafanyakazi hao ili usawa na haki ipatikane mahali pa kazi.

Naye Afisa programu Mwandamizi Masuala ya Utafiti Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Joyce Komanya amesema kwa mujibu ya ripoti iliyofanywa mwaka 2020/2021 inaonyeasha vitendo vingi vikiwemo ujira mdogo ajira za watoto wadogo mazingira hafifu ya utendaji kazi hali hiyo serikali haina budi kuingilia kati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com