Na Mwandishi Wetu
Katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi jamii imeshauriwa kuchangamkia fursa za Uwekezaji katika sekta ya Misitu nchini ili kuhakikisha wanalinda uoto wa Asili wa misitu pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya nchi.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa African Forest Kikolo Mwakasungura wakati wa Mkutano na Wadau wa uwekezaji wa sekta ya Misitu wanaoishi mijini .
Mwakasungura amesema kuwa Mkutano huo umelenga kuwakutanisha wadau wa Misitu hasa wanao ishi Mijini ili waweze kuchangamkiwa fursa ya kuwekeza katika sekta hiyo Muhimu nchini hasa maeneo ya Vijijini.
Aidha amesema kuwa kila mtu ana uwezo wa kuwekeza kwenye misitu hata kwa kuanza na hekalu moja.
"Suala la kuwekeza kwenye misitu ni la kila mtanzania na kwa hapa Nchini mikoa ya Nyanda za juu kusaini ndiyo sehemu zinazostawi zaidi ikiwemo Mbeya,Iringa,Songea,Njombe na Makete ni maeneo yanayostawi zaidi", alisema Mwakasungura.
Kwa upande wao baadhi ya Wawekezaji katika sekta ya Misitu waliohudhuria mkutano huo wameiomba Serikali kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ya Uchomaji moto wa Misitu ambayo kwa sasa imekisili katika Maeneo ya Vijijini.