Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU CCM ATOA SIKU 14 KWA VIONGOZI WA WILAYA NA MIKOA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza viongozi wa chama hasa kupitia Kamati za Siasa katika ngazi za wilaya na mikoa ndani ya siku 14 wakamilishe kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika maeneo yao na taarifa ya kilichojiri iwasilishwe ofisini kwake.



Sambamba na maagizo ya kuwataka kukagua miradi ya maendeleo, Chongolo pia amewaagiza kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani na amesisitiza kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.

Chongolo ametoa maagizo hayo tarehe 10 Agosti, 2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa  (SGR), akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekreterieti ya Chama Taifa.

"Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonesha njia nami nimeamka nije hapa na sekretarieti yangu kujionea kama kinachofanyika hapa ni kile kilichoelekezwa katika ilani yetu ya uchaguzi na ndicho kinachoelezwa kila mara,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ."

Amesema wao wanawajibu wa  kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani ni sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa  hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com