Kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake 3 katika Mahakama ya Kisutu imeahirishwa hadi 13 Agosti 2021, baada ya upande wa Serikali kudai taratibu za kuifungua kesi hiyo katika Mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza kutokamlika.
Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 asubuhi wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.
Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.
Social Plugin