Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara ACP Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea juzi katika kijiji hicho ambapo Philemon Tandu alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani shingoni karibu na nyumba yake baada ya mkewe Christina Elia (45) kumuacha akiwa na watoto watano akisema hamtaki tena.
Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni matatizo ya familia kwani mara baada ya Tandu kuachwa na mkewe walijaribu kusuluhisha ugomvi wao ili wasiachane na walee watoto wao ila ikashindikana mwanamke huyo akaondoka.
Social Plugin