Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTAKA : WAANDAENI WATUMISHI KABLA YA KUSTAAFU...WENGI WANATAPELIWA BAADA YA KUSTAAFU

Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka 

Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka ametoa maagizo kwa  Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) kuhakikisha kinasimama na wafanyakazi katika  kutetea maslahi yao pamoja na kuwaandaa watumishi wa Umma kujua nafasi zao mara baada ya kustaafu.

Mtaka amesema hayo  leo Agosti 24,2021 Jijini Dodoma katika mkutano Mkuu wa TALGWU  na kukitaka chama hicho kuendelea kutetea maslahi ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

"Mnapaswa kuwaandaa watumishi kabla ya kustaafu ili wajue wanatakiwa kufanya nini mara baada ya kustaafu kwani baadhi wamekuwa wakitapeliwa mara baada ya kustaafu," amesema.

Vilevile,amewataka kuwa na malengo yanayoishi ikiwemo kuweka vitega uchumi ambavyo vitawasaidia katika kujiendesha.

“Lazima muwe na malengo mnayoyaishi sio muda wote mpo Mahakamani hii inaharibu tengenezeni vitu vizuri ambavyo vitawaonesha,”amesema.

Pia amewataka kuwapa maelezo ya kutosha watumishi wapya ili wajue umuhimu wa Chama hicho kwani wengi wamekuwa wakidanganywa kuhusiana na chama hicho.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka kuwekeza Mkoani humo katika sekta ya ardhi kwani kuna fursa nyingi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TALGU Mkoa wa Mara, Dk.Magreth Shawu amesema wataendelea kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wafanyakazi ili wasikope mikopo   inayoumiza.

"Tutahakikusha tunatetea maslahi Kwa wafanyakazi Kwa maslahi ya Taifa,wafanyakazi wasipokuwa na migogoro wanakuwa na ufanisi mkubwa kazini,kwa kuanzia katika ngazi za mikoa tutaenda kulisimamia suala la utoaji wa elimu kwa watumishi wenzetu wasiyumbishwe akili kwa masuala yanayowaumiza ikiwemo  mikopo umiza,”amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com