Timu ya Arsenal imeambulia kipigo kwa mara nyingine baada ya kutandikwa mabao 5-0 dhidi ya Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika muda mfupi uliopita.
Mabao ya City yamewekwa kambani na Gundogan (dakika ya 7), Torres (dakika ya 12 na 84), Jesus (45) na Rodri (54) huku Xhaka wa Arsenal akiambulia kadi nyekundu.
Ni kipigo kingine cha maumivu kwa mashabiki wa Arsenal ambayo inashika mkia ikiwa imeruhusu mabao tisa katika mechi tatu na haijafunga bao hata moja!
Social Plugin