Kulia aliyekuwa Mbunge Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Jimbo la Konde visiwani Zanzibar Sheha Mpemba Faki (Picha kutoka mtandaoni).
Mbunge Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Jimbo la Konde visiwani Zanzibar Sheha Mpemba Faki amejiuzulu katika nafasi yake hiyo kutokana na changamoto za kifamilia.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka imethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu ya mbunge huyo leo, Agosti 2, 2021 kwa masikitiko makubwa.
Amesema Chama hakina uwezo kumzuia kwani ni haki yake ya msingi kama ilivyo haki yake msingi kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya ubunge ndani ya chama.
Sheha Faki aliibuka mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika jimbo la Konde baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Khatib Said kufariki.
Social Plugin