Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akimkabidhi majiko ya gesi Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Witness Makale ikiwa ni ishara ya kukabidhi majiko hao kwa kinamama wa UWT wa Wilaya , katika kikao kilichofanyika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akishuhudia Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Witness Makale akizindua pikipiki aliyomkabidhi kwa ajili ya mradi wa UWT Wilaya ya Nyamagana katika kikao kilichofanyika Ofisi ya CCM Wilaya ya Nyamagana leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akimkabidhi funguo ya pikipiki Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Witness Makale kwa ajili ya mradi wa UWT wa Wilaya hiyo ili kuinua kipato chao. katika kikao kilichofanyika Ofisi ya CCM Wilaya ya Nyamagana leo..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akikabidhi pikipiki na kompyuta kwa Mwenyekiti Jumuiya ya UWT Wilaya ya Ilemela Salome Kipondwa kwa ajili ya ofisi ya UWT, katika kikao kilichofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akimkabidhi jiko la gesi Mwenyekiti Jumuiya ya UWT Ilemela, Salome Kipondwa ikiwa ni ishara ya kukabidhi gesi hizo kwa wana jumuiya ya UWT Wilaya ya Ilemela katika kikao kilichofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akizungumza na wana Jumuiya ya UWT Wilaya ya Ilemela, kikao kilichofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
Baadhi ya kinamama wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Ilemela wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) alipofanya kikao na Jumuiya hiyo katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja akimkabidhi Mwakilishi wa Katibu wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Salama Mhampi fedha za miradi midogomidogo kwa ajili kinamama wa UWT Wilaya ya Nyamagana katika kikao kilichofanyika Ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana leo.
***********************
Na Mwandishi wetu-Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja amekabidhi kompyuta 2, mitungi ya gesi ya kupikia 100 na kuwawezesha kinamama wa Jumuiya za UWT Wilaya ya Ilemela na Nyamagana kuanzisha miradi midogomidogo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema pikipiki alizotoa zitasaidia kufanya shughuli ndogondogo ili wapate fedha zitakazoongeza mapato ya jumuiya hizo na kompyuta itasaidia katika uendeshaji wa shughuli za ofisi.
Akikabidhi majiko ya gesi ya kupikia Mhe. Mary Masanja amesema lengo ni kuwahimiza kinamama kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti hovyo na kuacha matumizi ya kuni na mkaa.
Aidha, Mhe. Mary Masanja amezihimiza jumuiya hizo kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki itakayowawezesha kuvuna asali ambayo itauzwa ndani na nje ya nchi.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Witness Makale amemshukuru Mhe. Mary Masanja kwa kuunga mkono juhudi za kinamama hao.
“Tunakushukuru kwa kutuunga mkono na kwa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais ya kutuhamasisha kutumia nishati mbadala ya gesi na tunakuahidi kutumia nishati hiyo ipasavyo.” amesema Bi.Makale.
Bi. Makale ameahidi kwa niaba ya wana UWT kuhakikisha wanafanyia kazi fursa alizozitaja za ufugaji nyuki, kutengeneza bidhaa za ujasiriamali kwa ajili ya kuwauzia watalii na kufanya fursa ya biashara ya bodaboda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Ilemela , Salome Kipondwa amempongeza Mhe. Mary Masanja kwa kupambana katika kuchapa kazi na kwamba wanajivunia kuwa na mwakilishi huyo bungeni.
Mhe. Mary Masanja yupo anaendelea na ziara yake ya kuzitembelembelea Jumuiya za UWT Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuzishukuru na kuzisaidia Jumuiya hizo zijikwamue kiuchumi.
Social Plugin