MISA -TAN YATOA MAFUNZO YA SHERIA KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.

Na George Binagi na Kadama Malunde - Mwanza
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja leo Jumamosi Agosti 28, 2021 katika ukumbi wa Hotel ya Victoria Palace jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.

Marawiti amezitaja Sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya Huduma za Habari , Sheria ya Takwimu na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA).

Amesema Waandishi wa Habari na Wahariri wakizifahamu vyema Sheria zinazosimamia taaluma ya Habari pamoja na Kanuni zake wataweza kutambua wajibu wao na kutimiza vyema majukumu yao huku wakizikabili changamoto zinazotokana na Sheria hizo.

Naye Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wahariri kuhusu mfumo wa sera za sheria za vyombo vya habari ili wasaidie kutumia nafasi zao kuleta mabadiliko kwa waandishi wa habari na jamii kwa manufaa ya taifa zima.

Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Jesse Kwayu amesema waandishi wa habari ni kundi la watu muhimu katika kutetea masuala mbalimbali ikiwemo sharia zinazokiuka haki za binadamu hivyo Waandishi wa habari wana jukumu la kulinda haki za binadamu na kuhakikisha haki za msingi zinalindwa.

“Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kulinda na kutetea haki za binadamu hivyo wawe mstari wa mbele kupigia kelele sheria zinazokiuka haki za binadamu na haki za msingi hazivunjwi wala kuingiliwa”,amesema Kwayu.

"Ni vizuri kuzijua sheria zilizopo katika tasnia ya habari ,tuzifuate kwani ukizijua sheria inakuwa rahisi kuzikwepa",aliongeza.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari leo Agosti 28,2021 jijini Mwanza. Picha na George Binagi na Kadama Malunde
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari
Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones akielezea lengo la mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu Sheria zinazosimamia taaluma ya habari
Mwezeshaji Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania

Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.

Mhariri wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwa ukumbini

Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na Maofisa wa MISA - TAN wakipiga picha ya pamoja

Picha na George Binagi na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post