KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusu kuelekea mkutano huo
MGOMBEA Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia akizungumza na Waandishi wa Habari leo |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema mkutano mkuu wa Kawaida wa Shirikisho ambapo moja ya agenda kubwa ni Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Jijini Tanga kesho
Ambapo maandalizi yake yakiwa yamekamilika kwa asilimia 95 ya wageni mbalimbali wakiwemo wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Africa CAF na Shirikisho la Soka Duniani FIFA wakitarajiwa kuhudhuria mkutano huo
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini hapa huku asilimia 5 ya wajumbe iliyobakia ikitarajiwa kuwasili leo kuungana na wenzao kwa ajili ushiriki wao.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Tanga Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wilfred Kidau alisema kwamba maandalizi yamekamilia huku wageni mbalimbali wakiwasili ikiwemo Rais wa Shirikisho la Soka nchini Somalia ambaye pia vilevile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Alisema pia walikuwa na kamati ua uchaguzi wa TFF kuhakikisha maandalizi ya muhimu yanakamilika wao kama sekretarieti ni wajibu wao kuhakikisha kamati ya uchaguzi ili iweze kufanya mambo yake kwa asilimia mia moja.
Alisema wapo wageni wengine mbalimbali wameanza kuwasilia Jijini Tanga ambapo wegine wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wakiwemo wajumbe wawili wawili wapo njiani tayari kutua Jijini Tanga.
Awali akizungumza na waandishi wa Habari Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema kikatiba kila baada ya miaka minne wanafanya uchaguzi na wa mwisho ulifanyika mwaka 2017 na safari hii wanafanya AgostI 7 wanafanya uchaguzi huo hapa jijini Tanga huku akiwaomba watanzania wawaombee kwa ajili ya mkutano huo.
Alisema kwamba mkutano huo utajadili taarifa zao za utekelezaji za mwaka na yeye atatoa taarifa yake ya miaka minne ya uongozi wake na wajumbe watajadili na baadae ya hapo wataenda kwenye uchaguzi huo anamshukuru Mwenyezi Mungu kwenye mkutano huo mgombea wa Urais atakuwa pekee yake na uthibitisho utafanyika kwenye mkutano huo hivyo anaomba wajumbe waweze kunithibitisha.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Biashara United ya Mara Selemani Mataso alisema uchaguzi huo ni muhimu sana hasa wao viongozi wa vilabu wanahitaji kupata watu ambao watawasaidia kuhakikisha wanaenda kutengeneza muonekano wa mpira ambayo haiwezi kuwa na shida na kuweka usawa wa vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza.
Alisema wakipatikana viongozi namna hiyo wakuangalia maslahi ya mpira inakwenda kutengeneza safu ya kuonyesha kwamba soka linakuwa linakwenda kujipambanua kuendesha soka la kisasa.
Social Plugin