Polisi katika kaunti ya Kiambu Ndumberi nchini Kenya wamemkamata mwanamke mmoja baada ya jamaa aliyekuwa akipalilia mgomba wakiwa kwenye chumba cha anasa kufariki dunia.
Wawili hao walikuwa katika chumba kwenye hoteli ya Konteina walipokuwa wakionja tunda la penzi.
Moses Muiruri aliamua kukodi chumba hicho baada ya wawili hao kuonja chupa kadhaa Ijumaa Julai 30,2021.
Duru kwenye mkahawa huo ziliambia gazeti la Standard kuwa wawili hao waliingia kwenye chumba nambari saba saa 4:30 asubuhi.
Kufikia Jumamosi Julai 31, kipusa huyo alijaribu kutoroka kutoka hoteli hiyo baada ya mambo kuenda sege mnege.
Polisi waliitwa baada ya Muiruri kupatikana kwenye chumba hicho akiwa amefariki dunia.
Mkuu wa polisi Ndumberi Badel Mohammed alisema mwendazake alipatwa akivuja damu kutoka mdomoni.
Kisa sawa na hicho kiliripotiwa Murang'a ambapo buda alizimia na kufariki dunia katika chumba alipokuwa na mpenziwe.
Frederick Opiyo alikuwa kwenye mkahawa wa Rurago saa tatu usiku Julai 27 akiwa na mpenzi wake Mary Mwende Munyalo kabla ya kuzirai na kuzima.
Mwende alisema alikuwa akuioga wakati ambapo aliskia dume huyo akiunguruma huku akiwa na matatizo ya kupumua.
Polisi walisema walifika katika eneo la mkasa na kupata vifaa vya kazi vikiwamo mipira ya kondomu na pia dawa za kuongeza nguvu za mapenzi.
Social Plugin