Mtoto anayedhaniwa kuwa mdogo zaidi ulimwenguni wakati wa kuzaliwa ameruhusiwa kutoka hospitali ya Singapore baada ya matibabu ya miezi 13.
Kwek Yu Xuan alikuwa 212g tu (7.47oz) – uzani wa tufaha – wakati alipozaliwa na alikuwa na urefu wa 24cm. Alizaliwa baada ya wiki 25 tu – badala ya kipindi stahiki cha wiki 40.
Aliyekuwa akishikilia rekodi ya zamani alikuwa msichana nchini Marekani ambaye alikuwa na uzani wa 245g wakati wa kuzaliwa mnamo 2018 kulingana na Usajili wa watoto wadogo wa Chuo Kikuu cha Iowa.
Mama wa Yu Xuan alimzaa kupitia upasuaji wa C section miezi minne kabla muda baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa ‘pre-eclampsia’ ambao ni shinikizo la damu hatari unaoweza kuharibu viungo muhimu na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto. Yu Xuan sasa ana uzani wa zaidi 6.3kg (paundi 14).
Social Plugin