MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14),akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 17 2021 akielezea jinsi alivyobuni Roboti ambayo itawasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani.
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14),akiwaonyesha vifaa vilivyotumika kubuni Roboti ambayo itawasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani waandishi wa habari , waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali,
Mwanafunzi wa Kidato cha sita, katika shule hiyo anaesomea masomo ya PCM, Oscar Mletwa,akizungumzia jinsi alivyobuni kifaa ambacho kitakuwa kikitoa taarifa kwa uongozi wa shule na Matroni mara baada ya kutokea kwa janga la moto.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ufundi Ifunda, Yusuph Mwagala,akielezea mafaniko na wanavyowaendeleza wabunifu hao kwa kuwakutanisha na Taasisi mbalimbali za ubunifu pamoja na Chama cha ubunifu na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) waandishi wa habari waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali,
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa wakielekea darasani
Muonekano wa majengo ya shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda iliyopo Mkoani Iringa iliyokarabatiwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
..........................................................................................
Na,Alex Sonna,Iringa
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi ya Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14) amebuni Roboti ambalo litakuwa likiwasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani lengo likiwa ni kumwepusha kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Pumu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 17,2021, waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali, mwanafunzi huyo amesema Roboti hilo litasaidia kusambaza dawa mashambani ili kuepuka mkulima kupata magonjwa mbalimbali.
“Nashiriki kutengeneza Project kwa kushirikiana na wenzangu ambalo litasaidia kupuliza dawa mashambani, nitatumia Roboti ambaye atasaidia kusambaza dawa katika mashamba ili kuepukana na kupata matatizo mbalimbali wakati wa kupulizia dawa,” amesema.
Amesema roboti hilo litatumia ramani ya shamba kwa kutumia Application maalum ambayo itakuwa katika simu ya mkulima.
“Application hiyo itakuwa katika simu ya mkulima ambayo atatumia ramani ya shamba na roboti atakuwa anazunguka katika shamba, itasaidia kuokoa muda ataenda shambani na kumuepusha na maradhi mbalimbali na magonjwa kama pumu.
William amesema roboti atakuwa kama kigari fulani na kutakuwa na tenki juu na kutakuwa na bomba na kwenye matairi kutakuwa na miyororo kama ya pikipiki kwa ajili ya kupita chini,”amesema.
Amesema itachukua muda wa wiki moja kukamilisha ubunifu huo ambapo amesema lengo ni kusaidia sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo cha kisasa.
“Serikali ina mapenzi ya dhati kuisaidia Serikali sisi kama wabunifu tutaiendeleza sekta ya kilimo na itasaidia sana katika sekta ya kilimo na mtu asiwe anapoteza muda,”anasema.
JANGA LA MOTO LAPATIWA UFUMBUZI
Katika hatua nyingine, Mwanafunzi wa Kidato cha sita, katika shule hiyo anaesomea masomo ya PCM, Oscar Mletwa amesema amebuni kifaa mbacho kitakuwa kikitoa taarifa kwa uongozi wa shule na Matroni mara baada ya kutokea kwa janga la moto.
Amesema kwa miaka mitatu 2019, 2020 na 2021 shule nyingi zimeungua moto ambapo amedai chanzo chake ni wanafunzi kujititengenezea shoti juu ya madari.
Alipoulizwa muda aliotumia kukitengeneza kifaa hicho, mwanafunzi huyo amesema ametumia miezi sita ambapo amedai malengo yake ni kuwa Mhandisi mkubwa nchini ili kuisaidia nchi katika mambo mbalimbali.
UBUNIFU WAO WAENDELEZWA
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ufundi Ifunda, Yusuphu Mwagala amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1950 na ina mchepuo wa ufundi kwa O level na A level kwa masomo ya Sayansi ambapo amesema katika masomo ya ufundi kuna ufundi wa ujenzi, umeme na mitambo.
Amesema kwa sasa wanaendelea kuwaendeleza wabunifu hao kwa kuwakutanisha na Taasisi mbalimbali za ubunifu pamoja na Chama cha ubunifu na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
Amesema mara baada ya kupata changamoto ya mabweni kuungua walipata wazo na kuwaomba wanafunzi kuwa wabunifu ili kubuni jinsi ya kukabiliana na majanga hayo.
“Ndivyo ambavyo wanafundishwa hivyo wamekuwa wabunifu tumepata changamoto ya mabweni kuungua tukapata wazo la kuwaomba wanafunzi mojawapo ni hii ya wanafunzi walifikiria namna ya kurahisisha kazi za mikono na mfumo wa kuzima taa kwa giza likiingia tu zinawaka na likiingia giza zinazima,”amesema.
Social Plugin