Mazishi ya mwili wa Hamza yakiendelea
Mwili wa Mwanaume aitwaye Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi katika makutano ya Barabara ya Kinondoni na Kenyatta Drive na kusababisha vifo vya askari wanne, watatu wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi umezikwa leo Jumapili Agosti 29 2021 saa 2 na nusu usiku katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es salaam baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga.
Mwili huo ulitarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana katika lakini msemaji wa familia Abdulrahm Hassan alisema mwili huo ulichelewa kutokana na kazi ya kutoa risasi zilizokwama.
Social Plugin